Jinsi Ya Kupika Bamia
Mchuzi wa bamia, ni mboga tamu inayopikwa kwa kutumia bamia mbichi, vitunguu, nyanya pamoja na viungo. Mboga hii yafaa kuliwa pamoja na ugali wali au hata chapati. Fiata hatua zifuatazo, ili ujifunze jinsi ya kupika mchuzi huu wa bamia.
Mahitaji
- 2 vijiko vya chai vya tangawizi iliyo twangwa
- ¼ kijiko cha chai cha binzari ya manjano
- ½ kikombe cha tui la nazi
- 1 kijiko cha chai cha vitunguu swaumu vilivyo twangwa
- 1 kiazi kikubwa cha mviringo kilicho menywa na kukatwa katwa
- 1 nyanya kubwa iliyo katwa katwa
- 1 kijiko cha chakula cha giligilani ya unga
- 1 kijiko cha chai cha binzari nyembamba ya unga
- 1 kijiko cha chai cha chumvi
- 6 vikombe vya bamia zilizo katwa katwa
- 2 vijiko vya chai vya mafuta ya kupikia
- 2 vijiko vya chakula vya tamarind paste
Hatua Za Mapishi
Hatua Ya 1
Chukua kikaango kikubwa chenye vijiko 2 vya chai vya mafuta ya kupikia na ukiweke kwenye jiko lenye moto wa wastani, kisha acha mafuta yapate moto. Weka bamia na uzikaange huku ukizigeuza geuza kwa muda wa dakika 8 mpaka 10, au hadi utakapo ona bamia zimebadilika rangi na kuwa na rangi ya kahawia. Epua bamia hizo na uziweke pembeni kwenye kontena.
Hatua Ya 2
Chukua mashine ya kusaga (blender). Weka kwenye hiyo mashine ya kusaga, tangawizi, vitunguu swaumu, nyanya, tui la nazi, tamarind paste, giligilani pamoja na binzari nyembamba, kisha saga hadi utakapo ona mchanganyiko huo umesagika vyema na kuwa laini.
Hatua Ya 3
Chukua sufuria kubwa lenye vijiko 2 vya chakula vya mafuta ya kupikia na uliweke kwenye jiko lenye moto wa wastani, kisha acha mafuta yapate moto. Weka ndani ya hiyo sufuria mchanganyiko ulio usaga kwenye mashine ya kusaga (blender), na upike mchanganyiko huo kwa muda wa dakika 7 mpaka dakika 10, au hadi utakapo ona mchanganyiko huo umebadilika rangi na kuwa na rangi ya kahawia.
Hatua Ya 4
Weka binzari ya manjano pamoja na chumvi halafu koroga vizuri, kisha weka viazi mviringo na upike huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa dakika 5.
Hatua Ya Mwisho
Weka maji, kisha funika sufuria na acha ichemke kwa muda wa dakika 5 mpaka 7, au hadi utakapo ona viazi vimeiva. Weka bamia na ukoroge vizuri, kisha funika tena sufuria na acha ichemke kwa muda wa dakika 5, au hadi utakapo ona bamia zimeiva. Epua mboga yako ya bamia na uweke pembeni, tayari kwa kula.