Jinsi Ya Kupika Biringanya za kuponda zenye njegere


Hatua Ya 1

Washa jiko la kuoka (oven) na uweke joto la nyuzi 205° C, kisha acha jiko lipate moto. Chukua mafuta ya kupikia na upake kwenye ngozi ya nje ya biringanya, kisha chukua kisu na uchanje sehemu mbali mbali za biringanya hizo kwa kutumia ncha ya kisu.

Hatua Ya 2

Weka biringanya ndani ya jiko la kuoka, kisha oka kwa muda wa dakika 30 mpaka 40, au hadi utakapo ona biringanya hizo zimekuwa laini. Ondoa biringanya hizo kutoka kwenye jiko la kuoka na uziweke pembeni ili zipoe.

Hatua Ya 3

Menya maganda ya biringanya hizo halafu ziponde vizuri, kisha ziweke kwenye kontena.

Hatua Ya 4

Chukua sufuria kubwa lenye mafuta ya kupikia na uliweke kwenye jiko lenye moto wa wastani, kisha acha mafuta yapate moto. Weka vitunguu maji kwenye hilo sufuria, kisha kaanga huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa dakika 5, au hadi utakapo ona vitunguu vimeiva.

Hatua Ya 5

Weka vitunguu swaumu, mbegu za giligilani, binzari nyembamba, garam masala, pamoja na chumvi, kisha kaanga huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa dakika 1.

Hatua Ya 6

Weka nyanya pamoja na majani ya giligilani, kisha pika mchanganyiko huo huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa dakika 5 mpaka 7, au hadi utakapo ona mchuzi wa nyanya umekuwa mzito.

Hatua Ya 7

Punguza moto na uweke moto mdogo. Weka biringanya ulizo ziponda pamoja na njegere, kisha pika mchanganyiko huo huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa dakika 15.

Hatua Ya 8

Mimina cream huku ukikoroga, halafu acha ichemke kwa muda wa dakika 1, kisha epua na upakue kwenye chombo safi, tayari kwa kula.
Next Post Previous Post
No Comment
Add Comment
comment url