Mapishi Ya Bagia Za Kunde
MAHITAJI
1.Kunde za bagia(kunde za kuparaza) robo kilo
2.Mafuta ya kupikia nusu lita
3.Vitunguu maji vidogo 4
4.Kitunguu thomu punje kubwa 10
5.Kotmiri kiasi
6.Chumvi kiasi
7.Pilipili Boga(Pilipili hoho) 1
8.Maji kiasi
-CHATNE
1.Nazi ndogo 1
2.Pilipili 1
3.Ndimu 1
4.Karoti ilokatwa 1
5.Pilipili boga(Pilipilihoho) lilokatwa 1
6.Chumvi
7.Maji
MAANDALIZI
1.Weka kunde kwenye ungo kisha zipete kuondoa uchafu
2.Loweka kunde zako kwa zaidi ya masaa 3
3.Kisha mwaga maji yote weka mengine
4.Anza kuzisafisha kunde zako mpaka zitoke maganda na vimawe vyote mpaka visafike
5.Menya Kitunguu Maji,Kitunguu Thomu Na Pilipili Boga
6.Kata vitunguu maji,pilipili boga,kitunguu thomu na kotmiri
7.Saga kwenye blenda kunde zako kisha weka chumvi na uzichanganye
8.Mimina Mchanganyiko wako weka kwenye bakuli
9.Weka chumvi na uchanganye vizuri
JINSI YA KUPIKA
1.Weka mafuta kwenye karai hakikisha yanapata moto kiasi
2.Anza kuchoma bagia kwa umbo upendalo.
3.Zikibadilika kuwa nyekundu geuza upande wa pili
4.Ziache ziive upande wa pili vizuri
5.Zitoe na uziweke kwenye chujio au tissue zichuje mafuta
6.Zikipoa kula na Na Juice au Chochote upendacho