Mapishi Ya Kachori
MAHITAJI
1.Viazi Mbatata Nusu.
2.Unga wa Ngano Kikombe Kikubwa 1
3.Mafuta Ya Kupikia Lita 1
4.Ndimu Kubwa 1
5.Pilipili za Kuwasha 2
6.Kitunguu Thomu Punje Kubwa 1
7.Chumvi Kiasi
8.Bizari Kijiko Cha Chai 1
9.Maji Kiasi
MAANDALIZI
1.Menya Viazi Mbatata katakata vipande na uvioshe
2.Weka kwenye sufuria na chumvi na maji kiasi
3.Twanga pilipili,kitunguu thomu na chumvi
4.Changanya unga,binzari na chumvi kiduchu
5.Weka maji kiasi kisha changanya kwa mkono
6.Hakikisha unapata uji mzito mzito
7.Kamua ndimu na maji kiduchu weka pembeni
8.Weka mafuta kwenye karai
JINSI YA KUPIKA
1.Vichemshe viazi vikiiva mwaga maji
2.Virudishe jikoni kwa sekende kadhaa vikauke kabisa
3.Ponda viazi vyako hadi viwe unga
5.Weka pilipili ulioitwanga na ndimu kwenye viazi na vichanganye kwa mkono hadi vichanganyike
6.Chukua mchanganiko wako tengeneza umbo la duara ukubwa uupendao
7.Weka mafuta jikoni yapate moto sana
8.Chovya maduara kwenye unga ulioweka binzari
9.Zungusha vizuri kisha tumbukiza kwenye mafuta ya moto
10.Acha ijishike usiwe na haraka ya kuigeuza
11.Ikijishika igeuze upande wa pili
12.Ukiona gamba la nje linakuwa gumu zitoe
13.Weka kwenye chujio zichuje mafuta
14.Acha zipoe kidogo tayari kwa kula
15.Unaweza kula zenyewe au na urojo,mkate,chatne n.k.