Mapishi Ya Katlesi Za Samaki
MAHITAJI
1.Viazi mbatata nusu(Vyenye Ngozi Ya Brown)
2.Samaki 4(Vibua)
3.Mafuta ya kupikia litre 1
4.Mayai 4
5.Keroti Kubwa 1
6.Ndimu 4
7.Kitunguu thomu punje kubwa 6
8.Chumvi kiasi
9.Tangawizi ndogo 1
10.Pilipili ya kuwasha 2
11.Paprika kijiko cha chakula 1
12.Unga wa mchele (Unga wa sembe au Bread crumbs)
13.Maji
14.Royco Paketi 1
MAANDALIZI
1.Osha Samaki muweke pembeni
2.Menya Viazi na vikate Kate weka pembeni acha na maji
3.Osha vitu vilobakia
4.Menya Tangawizi na Kitunguu thomu kisha vitwange na pilipili usiweke Chumvi
5. Vunja Mayai weka kwenye kibakuli na Chumvi kidogo yapige kama unataka kukaanga kisha weka pembeni
6. Chukua kibakuli na ukamue Ndimu na maji kidogo na ziweke pembeni
7.Para keroti yako weka pembeni
JINSI YA KUPIKA
1. Chemsha Samaki wako na Chumvi na Ndimu pamoja na Royco hakikisha haumkaushi anabaki na maji maji
2. Chemsha Viazi mbatata na Chumvi kiasi acha vichemke kisha vikiiva mwaga maji na rudisha jikoni kwa dakika 1 ili viwe vikavu kisha epua
3. Mtoe Samaki miba chukua nyama yake iweke Pilipili ulioitwanga changanya vizuri kisha weka pembeni
4. Chukua mwiko wa ugali au chupa ponda ponda vile Viazi ulivyo vichemsha mpaka vilainike vyote
5. Changanya Samaki,Viazi ulivyo viponda na keroti vizuri
6. Chukua donge la Viazi tengeza shape upendayo kisha nyunyizia Unga wa mchele kidogo juu ya katlesi zako
7. Weka mafuta jikon hakikisha yamekuwa ya moto sana chovya katlesi kwenye Mayai kisha weka kwenye karai
8. Acha kwa dakika 3 kisha zigeuze acha dakika kadhaa zikiwa na rangi ya dhahabu zitoe
9. Weka kwenye chujio au tissue zichuje mafuta zikipoa tayari kwa kula
10. Unaweza kula zenyewe au kwa chapati au na urojo