Simulizi Nzuri Ya Kusisimua: KID BOY Sehemu Ya 1
Simulizi Nzuri Ya Kusisimua Na Kuelimisha Pendwa Rika Zote KID BOY
Sehemu ya kwanza
Shughuli za shamba zikiwa zina endelea kwa kiasi kikubwa kwani ilikuwa ni wakati wa kutayalisha mashamba hashwa kwani msimu wa kilimo ulikuwa ume karibia sana.
Mama Sunday akiwa amembeba mtoto wake kipenzi Sunday mgongoni mwake huku akiendelea na shughuli za kusafisha na kukata vichaka, na kung’oa visiki maeneo ya shamba lake kwa bidii kubwa. Hekaheka zote zikiwa zinaendelea mtoto huyo akiwa tahabani kwa lindi kubwa la usingizi mgongoni kwa mamae.
Mama Sunday akiwa amechoka sana kwa kazi kubwa na jua aka shusha pumzi ndefu huku akifuta jasho kwa kipande cha kitenge kuu kuu alicho kuwa amevaa.... “Aaah! “ Taratibu akimshusha mtoto chini na kumlaza kwenye kipande cha kanga pale shambani pembeni yake na kisha akajilaza na kusema “ Pumzika mwanangu kipenzi cha roho yangu, pole na jua la mchana kutwa baba yangu” akasema mama Sunday huku akimlaza mtoto wake.
Baada ya dakika chache kupita akanyanyuka na kuji puputisha matataka yaliyo mjaa mwilini huku akitoa kibuyu cha maji na kunywa kwa mafundo kadhaa na kisha kuacha, huku macho yake yaki mtazama mtoto wake aliye lala pale chini na kisha kuangaza juu angani kuangalia jua linalo elekea kuzama.
Mama Sunday akiwa mchovu sana kwa kazi ya siku nzima aliyokuwa ame fanya.Taratibu akambeba tena mwanae mgongoni na kushika jembe, fundo la mboga kiunoni na kubeba jembe lake aki jikokota kuelekea nyumbani kwake.