Simulizi Nzuri Ya Kusisimua: KID BOY Sehemu Ya 2
Simulizi Nzuri Ya Kusisimua Na Kuelimisha Pendwa Rika Zote KID BOY
Sehemu ya Pili
Anafika nyumbani akamkukuta mdogo wake akimuandalia ugali na mlenda. Anakula kisha ana mnyanyua mwanae na kunyonyesha.
Haya yalikuwa ni maisha ya kila siku kwenye familia ya mtoto Sunday, na ndugu zake wawili pamoja na mama yao. Maisha yalikuwa ni magumu sana kwani hata kulala njaa ilikuwa ni kawaida sana kwao. Mama mzazi wa Sunday alikuwa ni mkulima mdogo mdogo wa mboga mboga na mazao ya biashara.
Hawakuwa na msaada wa ndugu wala jirani muda wote mama Sunday alipambana kupata chochote ili alishe familia yake na kusomesha watoto wake bila msaada wa mtu yoyote.
Kwa upande wa Sunday alikuwa na afya nzuri, muonekano mzuri sana japokuwa hakuwa na matunzo mazuri kivile. Na alikuwa ni mtoto wa kiume pekee katika familia ya mzee Madole, na maana ya neno Sande kwa lugha ya kigogo kiswahili chake ni asante. Kwa kuwa Sunday alikuwa ni mtoto wa kiume pekee kwao...baada ya kifo cha baba yao mzazi ndio alizaliwa mtoto huyo. Na mama yake aliamua kumpa hilo jina.
Mama Sunday aliolewa kama mke wa tatu kwenye enzi za uhai mzee Madole..wake wenza wa mama Sunday walikuwa ni watu wazima tu, lakini yeye aliolewa akiwa binti wa miaka kumi na tano.
.....subiri kujua chanzo cha kifo cha mzee Madole ni nini na je maisha yatakuwaje kwenye makuzi ya Sunday na hatima ya ndugu zake?!! ...