Simulizi Nzuri Ya Kusisimua: KID BOY Sehemu Ya 3
Simulizi Nzuri Ya Kusisimua Na Kuelimisha Pendwa Rika Zote KID BOY
Sehemu ya Tatu
Chanzo cha kifo cha mzee Madole ilikuwa ni utata mkubwa kwani alikufa ghafha, na tetesi kubwa ni uchawi. Na mtu pekee aliye shutumiwa ni mama Sunday kwani alikuwa ni kipenzi cha mzee Madole muda mwingi alikuwa akishinda na kulala nyumbani kwake.
Na ni mke pekee aliye pendwa kuliko wengine na enzi za uhai wa mzee Madole alikuwa ameweka wazi kusudio la kumrithisha mali.
Historia fupi ya mama Sunday, alizaliwa jijini Dodoma alisoma huko enzi za zamani hizo kabla haijawa jiji, masomo yake alisoma mpaka form five na six yaani elimu ya kidato cha tano na sita...wakati wa kumaliza masomo yake wazazi wake walifariki kwa ajari mbaya ya treni kipindi cha nyuma sana wakati walikuwa wana safiri kwenda Kigoma kwa bibi yake Sunday.
Mama yake Sunday aliitwa Edna Chikoya jina la usichana wake, kabila lake ni mgogo na mchanganyiko wa wa watu wa Kigoma.
Hali ya maisha ya awali ya mama Sunday yalikuwa ni mazuri sana kwani baba mzazi wa mama Sunday yaani, mzee Chikoya alikuwa ni mfanya biashara mkubwa mno, aliweza kumiliki maduka mengi na magari mengi makubwa ya kusafirisha mizigo ndani na nje ya nchi.