Simulizi Nzuri Ya Kusisimua: KID BOY Sehemu Ya 4

Simulizi Nzuri Ya Kusisimua: KID BOY Sehemu Ya 4

 

Simulizi Nzuri Ya Kusisimua Na Kuelimisha Pendwa Rika Zote KID BOY 


Sehemu Ya Nne

Ikiwa na pamoja na ununuzi wa mazao na uzaji wa mazao na bidhaa mbalimbali, pia aliweza kumiliki hotel kubwa na mengineyo. Hayo yalikuwa ni enzi za uhai wake ila vyote vilipotea tu wazazi hao walipo fariki, ndugu wa karibu na watu wa karibu walio kuwa wana simamia mali wali kimbiza na kuficha mali hizo. Ikiwa na pamoja na kunyanyasa watoto wa marehemu. 
      
Katika harakati za maisha na mwanzo wa uhusiano wa Mama Sunday yaani Edna na marehemu mume wake walikutana wakati bado anasoma na kwa muda ambao walianza mahusiano na ndoa... 

Wazazi wake Edna yaani mama Sunday alifukuzwa kwao wakati alipota ujauzito na kuvunja mahusiano kabisa na kwao..kwa upande wa mzee Mzee Madole alikuwa ni mtu wa kujiachia sana na mabinti wadogo haswa wanafunzi. 

Maisha ya mrembo Edna yalibadilika sana baada ya kumaliza shule na kukutana na maisha magumu ya mzee Madole aliye mpenda kwa muda wakati yupo nje lakini mambo yali badilika alivo muweka ndani na kuzalisha, matusi, kipigo ilikuwa ni kawaida sana kwa mama Sunday. Manyanyaso ya muda wote yalikuwa ni maisha ya kawaida..watoto wawili Sada na Silvia na Sunday.

👉👉Soma pia KID BOY Sehemu Ya 5👈👈

Next Post Previous Post
No Comment
Add Comment
comment url