Mheshimiwa Raisi Mama Samia Anatekeleza
Kazi anazofanya Rais mheshimiwa Dkt Samia Suluhu Hassan ni kubwa mno na zenye weledi wa hali ya juu, zinahitaji watu smart wenye uelewa makini wa mambo kumsemea kwa kuzielezea kwa mapana yake kwa jamii kwa weledi na kwa nidhamu pia kama namna ambavyo kazi hizo serikali imekuwa ikizitekeleza kwa weledi mkubwa.
Rais amefanya kazi kubwa sana kwenye mambo mbalimbali ila wimbi la vijana wanaojitokeza siku za karibuni kubuni mbinu mbalimbali za kila aina kujifanya wanamsifia na kumsemea Rais nadhan kwa upande mwingine wanakosea kwa kuzidisha mizaha na mbwembwe. Nashauri kazi za serikali zisemewe kwa weledi.
Mfano kero kubwa ya maji aliyoitatua Rais pale mkoani Shinyanga sidhani kama kunahitajika mwana tiktok maarufu wa vichekesho kumsemea mama kwa kazi ile iliyotukuka kwa kugalagala mitandaoni.
Vijana hawa wanaoibuka kujifanya wasifiaji kwa kugalagala na kila mbinu wanaharibu ubora wa ujumbe tarajiwa mbinu hizo kwa kiasi kikubwa zinaibua maswali kwa jamii yenye kuhoji na kutafakari kuna haja gani? Kiufupi nadhani hizi style za uchawa sio njia sahihi za kuzieleza kazi za Rais, nashauri vikundi hivyo vidhibitiwe. Hata nchi zilizoendelea kazi za serikali sio za kusemewa kwa namna ya mizaha na vichekesho ndio maana kuna mpaka idara za mahusiano na mawasiliano kwa ajili ya kueleza kazi hizo kwa weledi na mapana yake.
Nadhani wasomi, waandishi na vyombo vya habari vina nafasi nzuri ya kuzieleza kazi za Rais kwa umma kwa mapana yake na weledi zaidi, nadhani vipewe muongozo wa HABARI ZA KITAIFA ZA MAENDELEO NA UCHUMI ambapo vitakuwa vikiuhabarisha umma shughuli na miradi yote ya maendeleo inayotekelezwa na serikali yao kila siku angalau kwa dakika 20(Dakika 20 za Mama).
Wataalamu waalikwe na kueleza mafanikio ya serikali kwa mapana yake kwa jamii. Ni haki ya jamii kupata taarifa hizo muhimu kwa njia sahihi kujua namna serikali inavyofanya kazi kubwa kupitia kodi zao.