Ritha: Chanzo Cha Kuachana Na Diamond Ni Fantana
Kwa mujibu wa Ritha anadai chanzo cha kuachana na Diamond ni mwanadada Fantana wala sio Zuchu.
Baada ya Diamond Platnumz kudai kuwa Video zinazosambaa zikimuonesha akiwa na Mrembo Ritha ni za zamani kwamba ni zamiaka miwili nyuma 2023 na mwanamke huyo tayari amesha achana nae, Mrembo huyo amemjibu kupitia ukurasa wake wa Instagram kuwa Mwaka huo 2023 labda ndiyo mwanamke wake(Zuchu) aligundua kuwa wako pamoja.
Ritha ameandika kwamba;
"2023 ipi?? Labda unaongelea mwaka ambao msichana wako aligundua tupo pamoja hivo ukasugest tuwasiliane kwa number nyingine ili ajue tumeachana, mimi nmekuacha 2024 November, baada ya
Kuona Kisaikoloiia ndipo nikaamua kukutumia hiyo sms ya kukuacha baada yakugoma kulipa kodi.
"Mtu unaenikataza nisifanye kazi yoyote nikae tu ndani video call 24/7 af matumizi ya manati unaleta sababu Mia kidogo ukiambiwa
kodi ndio kabisa unakimbia kama sio wewe
ulienipangia iyo nyumba umecheza na akili yangu sana wewe na ndio tabia yako kucheza na akili ya mwanamke aliekupenda,
"Lakini nashukuru Mungu nilistuka mapema wewe mtu mkubwa na pesa bieberi nishinda ukitumia ivo vigezo lakin ukweli unaujua umeninyanyasa sana tumeenda south Unalalala na mwanamke mwingine
chumba kingine ambaye ni fantana mi unaniacha chumbani kisa nipo kwenye siku zangu za mwezi arafu nakuuliza why umefanya ivo unanigeuzia kibao.
"Mimi ndio ninamakosa eti nakusingizia wakati kitanda kinaonesha mmefanya mambo yenu mimi siwezi kukublackmail wewe hata siku moja nimekusema nini mimi siwezi video kama ningeuza basi ningeuza zote nilizonazo kwenye simu kwanini niuze nusu kilichotoke unakijua wewe mwenyewe na mambo yako nimesikitishwa sana kuhusishwa na pia sitaki huo uzalilishaji wako unaonifanyia"
Hayo ni maneno ya mrembo Ritha aliyekuwa mpenzi wa siri wa Diamond Platinumz.