Simulizi Nzuri Ya Kusisimua: KID BOY Sehemu Ya 5

Simulizi Nzuri Ya Kusisimua: KID BOY Sehemu Ya 5

Simulizi Nzuri Ya Kusisimua Na Kuelimisha Pendwa Rika Zote KID BOY

Sehemu Ya Tano

Edna anakuwa njiapanda baada ya kifo cha mumewe na anaamua kujitenga na maisha yake ya zamani. Akapata dhuruma kubwa ya mali za mumewe, ikawa ni kesi juu ya kesi akakosa vyote mume na hata mali zake.

Na hapo hapo Straton anakuwa yupo mbali naye hivi karibuni baada ya kujua Edna ni mjamzito na ukizingatia yeye alishaoa huko Marekani na alikuwa na familia kabisa hivyo aliamua kutorudi na kukata mawasiliano na mpenzi wake wa zamani.

Uzuri wa mrembo Edna ambaye sasa akiwa ni Mama au binti wa miaka ishirini na tano tu! akawa ni mjane na mwenye watoto watatu kwa mpigo. Huku wanae wakubwa Sada na Silvia wakiwa na miaka saba kwa wakati huo na pia mdogo wao Sunday akiwa na miaka miwili.

Maisha yalimfanya Edna awe mbaya kwa kufubaa ngozi yake nyeusi na nzuri yenye kutereza, shepu na mvuto wake. Ikiwa ni pamoja na hipsi na makalio yake makubwa kuisha kabisa na kuwa miss, akaonekana kama mzee kwa uchovu wake wa kuzaa haraka haraka na kukosa matunzo mazuri na hakuna kitu kilicho muumiza na kumkondesha kama mawazo.

Mawazo kwake yalikuwa ni kawaida sana kwani aliwaza mengi sana moja wapo ni maisha ya baadae ya wanae watatu ambao walimtegemea sana Mama yao. Hali yake ya kiuchumi ilikuwa ni ngumu hakupata pesa zaidi ya Elfu kumi na alijitahidi kadri ilivyowezekana akawapeleka watoto wake Shule.

Je? Nini kitatokea kwa Edna na watoto wake, usiache kusoma mwendelezo mwengine wa simulizi hii...


👉🏽👉🏽👉🏽Soma pia sehemu ya 6 hapa👈🏽👈🏽👈🏽

Next Post Previous Post
No Comment
Add Comment
comment url