Simulizi Nzuri Ya Kusisimua: KID BOY Sehemu Ya 6
Simulizi Nzuri Ya Kusisimua Na Kuelimisha Pendwa Rika Zote KID BOY
Sehemu Ya Sita
Japokuwa ilikuwa ni mwanzo mgumu, kwa vile vilihitajika vitu vidogo vidogo kama vile sare za shule, madaftari na michango mbali mbali ya shuleni. Na ukizingatia shule nyingi za msingi zinakuwa na michango kibao isiyo na mpangilio kama fedha kwa ajili ya madawati au mlinzi na mingineyo kibao.
Yote hayo hayakuweza kumudiwa, ua Edna hakuweza kuyamudu hata kidogo zaidi ya kuomba msaada kwa watu. Ikafika kipindi hakwenda shambani alilazimika kwenda mjini na kuomba omba barabarani na kwenye majumba ya watu.
Edna aliona njia mbadala ya kujiokoa maisha yake ni kwenda kuomba omba na kujipatia visenti vya kuweza kulipia na kununua mahitaji ya wanae. Ikiwa ni miaka mitatu baadae hile tabia ikakomaa na kuota mizizi kabisa, Edna hakujali kuona watu waliomfahamu kama mtoto wa mfanyabiashara mkubwa kukaa barabarani na kuomba omba.
Yeye alichowajibu ni kwamba hiyo ni historia kwani Baba yake na Mama yake walishafariki siku nyingi sana hata hajui mali yoyote aliyoachwa basi ikawa watu wakaanza kumkwepa waliomfahamu enzi hizo, wenye huruma walimsaidia.
Ikawa anapata vibarua na kujipatia pesa nzuri kiasi cha kumtosheleza mahitaji yake na wanae. Na kwa wakati wote huo alimchukua Sunday na kwenda naye kuomba omba. Hivyo ile tabia ikaanza kumuingia Sunday akiwa mtoto mdogo wa miaka mitano tu!
Nini kitatokea? tukutane kwenye mwendelezo mwingine wa Simulizi hii...