Simulizi Nzuri Ya Kusisimua: KID BOY Sehemu Ya 7
Simulizi Nzuri Ya Kusisimua Na Kuelimisha Pendwa Rika Zote KID BOY
Sehemu Ya Saba
Maisha yakaendelea, Sada na Silvia wakiwa wanasoma darasa la nne hivi, walikuwa wanakerwa sana na tabia ya Mama yao na walimuonya Mama yao kwa tabia hile. Lakini Edna aliona kuwa ni raha na akawa mvivu na kuacha kabisa kushika jembe. Maisha yakawa maguu zaidi, ikafika kipindi Edna alirudi nyumbani mikono mitupu. Edna alikuwa amefanya zuzu bila kujielewa.
Atari zake zilikuwa zimeshikwa na mke mkubwa wa marehemu mumewe. Visa vilizidi mno na mbaya zaidi, yule mwanamke akazidisha vidawa hili kusambaratisha familia na zaidi kusimamisha maendeleo ya familia ya kina Sunday.
Mambo yakaanza kuharibika taratibu wale watoto wakina Sada na Silvia wakaacha shule na kufatana na Mama yao kuomba omba mjini huku Sunday naye akiwa kibaka mtoto na chokoraa wa kutupwa, ikafikia kipindi alitoroka na kuwa kimbia ndugu zake. Hapo ndio chanzo cha kisa cha kusisimua cha maisha ya familia ya kina Sunday na utengano wao.
Sunday anaingia kitaa na kuanza kusumbua Jiji kinoma noma. Akiwa na umri mdogo tu! akaanza na kujihusisha na vitendo haramu vya wizi na udokozi. Waliliza watu hile kichizi wakafanya kila aina ya uchafu wa mitaani. Na ikiwa baada ya miaka mitano baadae anakamatwa na kuwekwa ndani kwenye jera ya watoto.
nini kitatokea baada ya Sunday kwenda Jera? endelea kusoma muendelezo mwingine...