Simulizi Nzuri Ya Kusisimua: KID BOY Sehemu Ya 9

Simulizi Nzuri Ya Kusisimua: KID BOY Sehemu Ya 9Simulizi Nzuri Ya Kusisimua Na Kuelimisha Pendwa Rika Zote KID BOY 

MTUNZI: Lucy Vincent

Sehemu Ya 9

Kwa vile Sunday alikuwa na hamu ya pesa akawa anamuoshea gari Cindy kwa muda wa wiki kadhaa hivi. Ikawa siku moja Cindy akiwa kwao mitaa ya AREA 'D', ametulia akiwa anaangalia filamu kwenye laptop yake akapigiwa simu na best yake aitwae Angel watoke kwani wanabonge la mtoko na sharobaro mmoja hivi.

"Listen Darling, mm siwezi kutoka mpenzi because i have alot of thing's to take care of" akasema Cindy kwa pozi. Angel akashusha pumzi, upande wa pili wa simu " acha hizo best mimi nishaongea na Ray kuhusu mtoko wa leo si unajua tuliongea nini siku ile pale Golden Crown please, usitake kuniangusha, mimi nishaongea nae na amesema yupo on is way kwangu na soon atafika, so itakuwaje na atachuliaje mi siwezi kumplease Raymond ampaka akubali si! unajua anavyopenda kampani" Akasema Angel kwa sauti ya ukali na pozi za kihela hela.

Cindy kwa pozi zaidi " come on Girl, mi! leo sijisikii kutoka kama unaweza toka nae" akasema Cindy na kukata simu kwa haraka, kiasi cha kumpa sintofahamu best wake huyo.
"Mmmh" Akashusha pumzi Cindy huku akibofya simu yake kumpigia simu Raymond "hellow, dia mambo" Akasema Cindy kwa pozi za kijanja na uchokozi mno. "safi tu mpenzi mi! nipo poa nakaribia kufika kwa kina Angel vipi upo nae au bado upo Home?" Akauliza Raymond.

Tukutane tena kwenye episode nyingine ya Kid boy...


👉👉Soma pia KID BOY Sehemu Ya 10👈👈

Next Post Previous Post
No Comment
Add Comment
comment url