Simulizi Nzuri Ya Kusisimua: KID BOY Sehemu Ya 11
Simulizi Nzuri Ya Kusisimua Na Kuelimisha Pendwa Rika Zote KID BOY
MTUNZI: Lucy Vincent
Sehemu Ya Kumi Na Moja
Wakasalimiana na kisha akamkaribisha "karibu shem, vipi mbona umechelewa sana don't tell me Dom kuna foleni kiasi cha kukuchelewesha" Akauliza Angel kwa utani. Wote wakacheka na kisha akasema " Niambie shem, umeshaongea na Cindy?" Akauliza tena Angel kwa mshangao " kuhusu hile issue, bado amenizingua kishenzi mi! simuelewi siku hizi emabadilika sana vipi, kwani kuna nini kinaendelea shem!" Akasema Raymond.
"hamna shem lakin mi! ameniambia hayuko sawa hawezi kutoka leo" Akasema Angel, Raymond akajibu " sio leo tu, nafikiri kati ya hizi wiki mbili amebadilika mno amepunguza upendo Cindy wa zamani si! Cindy wa sasa" Angel akashusha pumzi na kusema " usijali shem, nitaongea nae natumaini atanielewa tu" akamtia moyo shemeji yake. "Dah! sawa shem hebu ngoja nirudi chuo si unajua nimetoroka kipindi chuoni" Akasema Raymond huku akinyanyuka Angel akamsindikiza shemeji yake mpaka nje mahari alipoegesha gari lake.
Raymond akasisitizia kuhusu Cindy, Angel akamtoa shaka juu ya hilo na kumuahidi kila kitu kitaenda sawa. Raymond akaondoka na kurudi chuoni huku nyuma Angel akampigia shosti na kumuuliza kulikoni. "kwanini umemfanyia hivyo best friend kwani tatizo ni nini!?" Akauliza Angel kwa mshangao, Cindy akasema " hakuna tatizo lolote, ukweli ni kwamba sijisikii hata kidogo kutoka out na Ray". Angel akaishiwa pozi kwa jibu la shosti wake huyo mwenye pozi nyingi.
Itaendelea...