Simulizi Nzuri Ya Kusisimua: KID BOY Sehemu Ya 12
Simulizi Nzuri Ya Kusisimua Na Kuelimisha Pendwa Rika Zote KID BOY
MTUNZI: Lucy Vincent
Sehemu Ya Kumi Na Mbili
Cindy anapomaliza kuongea na Angel akanyanyuka kutoka kitandani na kusimama mbele ya kabati la nguo na kuchagua viwalo vikali na kuchomoka na kisha kushuka mpaka sitting room na kumkuta mdogo wake wa kiume aitwaye Jason na kumwambia " Jason mi! natoka kama utahitaji chochote utanipigia, na kama mtu yoyote akija kuniulizia mwambie nimetoka kidogo sawa?" Akasema Cindy.
Jason akasema "Lakini Sisy......kabla ya kumaliza sentensi. Cindy akamzuia kuendelea kuongea na akamwambia kwa sauti ya chini "shiiiii...nisikilize nikuletee nini nikirudi?" Akauliza Cindy huku akichuchumaa pembeni ya sofa alilokaa Jason. Jason huku akikunja uso wake " nitamwambia Dady na Mumy kila kitu, si uliambiwa uniangalie kwanini uniache sasa hapa, twende wote" akasema Jason. Cindy akashusha pumzi na kisha akasema "sawa twende nenda kajiandae twende zetu". Jason akarukaruka kwa furaha, akiwa ni mtoto mdogo wa miaka mitano hivi. Jason akapanda mpaka chumbani kwake kwenda kuvaa, huku nyuma Cindy akamwambia yule housegirl wao " Please, muangalie Jason asiondoke kabisa"
Akaondoka kwa haraka huku akiendesha gari lake, kuelekea mitaa ya Chadulu mtaa ambao anaishi Sunday. Anafika kijiweni anamuulizia Sunday akaambiwa ametoka kidogo. Hivyo akampa ofa mtu mwingine amuoshee gari lake. Wakati akiwa amesimama pembeni, Sunday akafika.
Itaendelea...