Simulizi Nzuri Ya Kusisimua: KID BOY Sehemu Ya 8
Simulizi Nzuri Ya Kusisimua Na Kuelimisha Pendwa Rika Zote KID BOY
MTUNZI: Lucy Vincent
Sehemu Ya Nane
Anakaa ndani kwa muda mrefu sana hadi anapofikisha miaka kumi na tano anaachiliwa na kuingia mitaani. Akiwa na mtazamo mpya wa maisha yake na anaona ni bora atafute kazi yoyote afanye na kujipatia kipato cha kila siku. Sunday anaamua kutafuta kazi bila mafanikio, kwani kila alipoenda alikataliwa kwa uchafu wake ambao alikuwa amefanya kipindi cha nyuma na afya yake mbaya aliyokuwa nayo.
Ngozi yake ilichakaa ukurutu na mapunye na majipu kwa wingi. Sunday alikuwa ni mchafu wa kunuka hivyo akafanya janja ya nyani na kupata sabuni na maji na kuoga na kufua nguo zake. Anabadilika mno na kuvutia kiasi fulani, Sunday akawa ni kijana mzuri na mwenye mvuto mno japokuwa alitoka kwenye mazingira magumu sana na ya matatani sana, hakuna asilolijua katika maisha kwani alikuwa na elimu ya kitaa zaidi japokuwa hakuwahi kukaa darasani na kusoma ila alijua mbinu zote za kupata pesa mjini kwahiyo haikuweza kupita siku bila kula chochote pale mjini.
Siku moja katika pitapita zake akakutana na demu mmoja wa kishua, ambaye alikuwa ni mrembo sana na alijulikana kwa jina la Cindy ambaye alionekana ni binti wa miaka kumi na tano hivi. Cindy akampa dili Sunday amuoshee gari lake gari lake kali sana la kifahari.
Je nini kitatokea baina Sunday na Cindy? tukutanane katika kipande kinachofata