Simulizi Nzuri Ya Kusisimua: KID BOY Sehemu Ya 10
Simulizi Nzuri Ya Kusisimua Na Kuelimisha Pendwa Rika Zote KID BOY
MTUNZI: Lucy Vincent
Sehemu Ya Kumi
Kwa sauti nyororo na pozi za kizungu, "No, my love" Akajibu Cindy, Kwa upande wa Raymond "Why not? si! unajua mda umeenda sana mpenzi na baadae nitachelewa kurudi chuoni" Akasema Raymond kwa mshangao mkubwa. "listen my love, Leo sijisikii vizuri na isitoshe Mom and Dad hawapo nyumbani nimebaki mimi tu na mdogo wangu na nimeambiwa nimuangalie asitoke so, wewe unadhani itakuwaje mpenzi?" Akajitetea Cindy kwa sauti ya mahaba zaidi.
"Okay nimekuelewa but umenimaliza mafuta bure ningejua mapema nisingekuja" Akazidi kulalamika Raymond. Cindy akasema "wala usihofu kwani huwezi kutoka na Angel?" akauliza Cindy. Raymond akamjibu "naweza, but wewe ndio mlengwa mpenzi, umeniangusha mno mi! nimeacha kipindi kwa sababu yako ujue" Akalalamika Raymond. Cindy akamwambia " Don't worry ma love, next time nitakujulisha as soon as possible" Raymond akashusha pumzi ndefu na kisha akasema "anyway nitakupigia baadae kuna issue nataka kukueleza" Akasema Raymond
Baada ya kuongea na simu akawa ameshafika round about ya ZUZU na kisha akakatisha kupandisha juu kuelekea Uzunguni. Anapofika anapokelewa na Dada yake Angel mpaka ndani ambako anamkuta Angel akiwa anafanya maswali yake aliyopewa shuleni.
Itaendelea......