Hassan Mwakinyo atupwa rumande kwa kesi ya kushambulia wezi wa nazi
Pichani ni bondia wa Tanzania Hassan Mwakinyo akiwa na bondia Terrence Crawford wa Marekani mwaka 2022 alipokuwa nchini humo (Marekani) na kupata fursa ya kufanya mazoezi na mabondia wa nchi hiyo kwenye gym maarufu.
Kwa sasa Terrence Crawford ni bingwa wa dunia asiyepigika (undisputed world champion) Wakati Hassan Mwakinyo yupo rumande kwa kesi ya kushambulia wezi wa nazi, nazi hizi wanazotumia wachawi kurogea kututupia majin nazi hiz mama ntilie wanazotumia kuungia mboga. Nazi za jero jero.
Hapa ndio tunasema kuna umuhimu mkubwa wizara ya michezo kuzipa nguvu taasisi na makampuni makubwa yanayosimamia vipaji kuvipa thamani na hadhi halisi, wadau hao ni muhimu mno katika kuendeleza, kutangaza na kuvipa thamani vipaji nchini.
Mwakinyo angekuwa na Management nzuri angekuwa bondia tajiri wa level za kidunia leo.
Vipaji vingi bado vinaishia kwenye maisha ya kipuuzi kabisa kwa kukosa management thabiti.