Nicole Berry Kabla na baada ya kutupwa Lupango kwa tuhuma za utapeli
Pichani ni mrembo Nicole Berry Kabla na baada ya kukamatwa kwa tuhuma za utapeli, unaweza kudhani ni watu wawili tofauti kabisa aisee.
Binafsi niseme maisha wanayoishi watu wengi mitandaoni hususan insta sio halisi yana siri nyingi, vijana wengine wanapakwa mafuta nk kuna mzee mmoja aliwahi kuniambia ukiona mtu anaishi maisha ya kifahari usitamani sana akikwambia yaliyo nyuma yake unaweza kuona umaskini wako ni jambo la kheri kabisa.
Wasanii na wanamitandao wengi wametawaliwa na maisha feki ya kitajiri ila kiuhalisia ni watu wa kawaida kabisa.
Nampa pole sana dada huyu, mapito haya yawe fundisho kwa wengine.