Rais wa Marekani Donald Trump kuwachimba mkwara Iran
Rais wa Marekani Donald Trump amemtumia barua kiongozi mkuu wa Iran Ayatollah Ali Khemenei akiitaka Iran kukubali mpango mpya wa mazungumzo ya kusitisha utengenezaji wa silaha za nyukria unaopendekezwa na Marekani, Trump katika barua hiyo ameitaka Iran kukubali mazungumzo ya kusitisha mpango wa nyukria kwa hiari au ilazimishwe kijeshi.
Kiongozi mkuu wa Iran Ayatollah Ali Khemenei amelaani barua hiyo na vitisho hivyo vya Trump na kusema kamwe Iran haiwezi kushurutishwa kufanya mazungumzo na taifa lolote.
Juma lililopita vyombo vya habari vya kimataifa wakiwemo Reuters viliripoti taarifa za Iran kuwa katika mazoezi makali ya kijeshi ya utayari ya kivita yaliyoanza mwezi Desemba mwaka jana kufuatia kitisho kikubwa cha maeneo yake ya kimkakati ya uzalishaji wa nyukilia kushambuliwa na Marekani na Israel jambo ambalo Iran imesema litasababisha vita kubwa.
Tayari Marekani imeimarisha maradufu vikwazo vikali vya kiuchumi dhidi ya Iran na serikali ya rais Trump inatarajiwa kuongeza zaidi vikwazo. Katika mkutano uliofanyika nchini China wiki hii kuhusu mpango wa nyuklia wa Iran uliokutanisha China, Urusi na Iran mataifa hayo yamelaani vikwazo vya Marekani yakiviita kandamizi. Hali ya uchumi katika taifa hilo la ghuba ipo kwenye mkwamo uliosababisha baadhi ya viongozi wa juu kujiuzulu.
Mapema mwaka huu rais wa Ufaransa Emmanuel Macron alionya kwamba Iran inakaribia kuunda silaha za nyuklia na hivyo kitisho hicho sio cha kupuuzwa hata kidogo kwa maslahi mapana ya Dunia.
Ikumbukwe Israel imeapa kwamba kamwe haitoruhusu Iran imiliki silaha za nyukria. Wiki iliyopita shirika la habari la Marekani la New York Post liliripoti kwamba kuna uwezekano mkubwa Israel ikashambulia miundombinu ya nyukria ya Iran katikati ya mwaka huu .
Mataifa hayo ni mahasimu wakubwa wa miaka mingi.
Je Iran itafanikiwa kumaliza 2025 bila kuvamiwa?